2 Timothy 2

1Kwa hiyo, wewe mwanangu, utiwe nguvu katika neema iliyondani ya Kristo Yesu. 2Na mambo uliyoyasikia kwangu miongoni mwa mashahidi wengi, uyakabidhi kwa watu waaminifu ambao wataweza kuwafundisha wengine pia.

3Shiriki mateso pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu. 4Hakuna askari atumikae wakati huo huo akijihusisha na shughuli za kawaida za maisha haya, ili kwamba ampendeze ofisa wake mkuu. 5Pia kama mtu akishindana kama mwanariadha, hatapewa taji asiposhindana kwa kufuata kanuni.

6Ni Muhimu kwamba mkulima mwenye bidii awe wa kwanza kupokea mgao wa mazao yake. 7Tafakari kuhusu nisemacho, kwa maana Bwana atakupa uelewa katika mambo yote.

8Mkumbuke Yesu Kristo, kutoka uzao wa Daudi, ambaye alifufuliwa kutoka kwa wafu. Hii ni kulingana na ujumbe wangu wa Injili, 9ambao kwa sababu ya huo ninateswa hata kufungwa minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu halifungwi kwa minyororo. 10Kwa hiyo, navumilia mambo yote kwa ajili ya wale ambao Mungu amekwishawachagua, ili kwamba nao pia waupate wokovu ulio katika Kristo Yesu pamoja na utukufu wa milele.

11Usemi huu ni wakuaminika: “Ikiwa tumekufa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia, 12kama tukivumilia, tutatawala pamoja naye pia, kama tukimkana yeye, naye pia atatukana sisi. 13kama hatutakuwa waaminifu, yeye atabaki kuwa mwaminifu, maana hawezi kujikana mwenyewe.”

14Endelea kuwakumbusha juu ya mambo haya. Waonye mbele za Mungu waache kubishana kuhusu maneno. Kwa sababu hakuna manufaa katika jambo hili. Kutokana na hili kuna uharibifu kwa wale wanaosikiliza. 15Fanya bidii kujionesha kuwa umekubalika kwa Mungu kama mtenda kazi asiye na sababu ya kulaumiwa. Litumie neno la kweli kwa usahihi.

16Jiepushe na majadiliano ya kidunia, ambayo huongoza kwa zaidi na zaidi ya uasi. 17Majadiliano yao yatasambaa kama donda ndugu. Miongoni mwao ni Himenayo na Fileto. 18Hawa ni watu walioukosa ukweli. Wanasema ya kuwa ufufuo tayari umishatokea. Wanapindua imani ya baadhi ya watu.

19Hata hivyo, msingi imara wa Mungu unasimama, wenye uandishi huu, “Bwana anawajua walio wake, na kila alitajaye jina la Bwana ni lazima ajitenge na udhalimu.” 20Kwenye nyumba ya kitajiri, siyo kwamba vimo vyombo vya dhahabu na shaba tu. Pia kuna vyombo vya miti na udongo. Baadhi ya hivi ni kwa ajili ya matumizi ya heshima na baadhi yake ni kwa matumizi yasiyo ya heshima. 21Ikiwa mtu atajitakasa mwenyewe kutoka kwenye matumizi yasiyo ya heshima, yeye ni chombo chenye kuheshimika. Ametengwa maalumu, mwenye manufaa kwa Bwana, na ameandaliwa kwa kila kazi njema.

22Zikimbie tamaa za ujanani. Ukifuata haki, imani, upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi. 23Lakini ukatae upumbavu na maswali ya kipuuzi. Kwani unajua ya kuwa huzaa ugomvi.

24Mtumishi wa Bwana hapaswi kugombana, badala yake inampasa kuwa mpole kwa watu wote, awezaye kufundisha, na mvumilivu. 25Ni lazima awaelimishe kwa upole wale wampingao. Yamkini Mungu aweze kuwapatia toba kwa kuifahamu kweli. Waweze kupata ufahamu tena na kuepuka mtego wa Shetani, baada ya kuwa wametekwa na yeye kwa ajili ya mapenzi yake.

26

Copyright information for SwaULB